ZINAZOVUMA:

Ubora wa elimu vyuo vikuu wapungua

Ubora wa elimu wa vyuo vikuu unatajwa kuwa kwenye hatari...

Share na:

Ubora wa elimu ya vyuo vikuu nchini unatajwa kuwa kwenye hatari kutokana na uhaba wa wahadhiri.

Baadhi ya wadau wa elimu wametoa maoni juu ya takwimu mpya zilizotolewa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) walisema jitihada za haraka zinatakiwa kufanyika kunusuru sekta ya elimu ya juu.

Takwimu hizo zinaonyesha bado idadi ya wahadhiri wanaotambulika na taasisi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi wa ngazi hiyo.

Takwimu hizo zilizotolewa na ripoti ya ‘Vitalstats 2022’ zinaonyesha wahadhiri na wafanyakazi wengine wa kitaaluma katika taasisi za elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2022/23 ni 8,507, huku wakihudumu katika kada 17 na programu mbalimbali 2,160 katika vyuo hivyo.

Kwa mujibu wa muongozo wa elimu ya juu toleo la mwaka 2019 kilichotolewa na TCU, kwa masomo ya sanaa na sayansi ya jamii wastani wa mhadhiri mmoja anapaswa kufundisha wanafunzi 50.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya