ZINAZOVUMA:

Tusiruhusu maharamia kwenye soka.

Mkurugenzi wa sheria wa Yanga amesema kama mchezaji anataka kuvunja...

Share na:

“Hatumng’ang’anii Feisal lakini tunataka utaratibu ufuatwe. Kama tutaruhusu Feisal kuondoka kwa njia hii, kuna siku hatutakuwa na mpira maana mchezaji ataamka asubuhi na atasema hana furaha basi anaondoka”

“Huu ni uhuni ambao hautakiwi kuruhusiwa katika mpira. Ziko njia rasmi za kuvunja mkataba na zinafahamika hadi (FIFA)”

“Tunachotaka kanuni za mpira zisimamiwe, tusiruhusu MAHARAMIA wanaotumia fedha. Ikitokea wameruhusu hili nina hakika kabla msimu haujaisha atatokea mwenye fedha atawajaza Mamillioni atawaambia andikeni barua hamna furaha poteeni baadae mtaomba kuvunja mikataba mtaruhusiwa.. Na hii sio kwa Yanga tu klabu zote”

“Sisi tunachokitaka sheria na taratibu zifuatwe, sisi hatuwezi kumruhusu aondoke kiholela japo sio kwamba tunamng’ang’ania. Akifuata Utaratibu TUTAMRUHUSU AONDOKE, Yanga ni kubwa kuliko mtu yeyote”

▪️ Esq. Simon Patrick
Mkurugenzi wa sheria Yanga via Clouds Fm

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya