ZINAZOVUMA:

“Tumeimarisha mahakama ili kuondoa mlundikano wa kesi”

Raisi Samia Suluhu Hassani amewataka majaji walioteuliwa na kuapishwa wakatende...

Share na:

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka majaji kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia misingi ya kutoa haki kwa kila mmoja bila upendeleo kama ambavyo wameaminiwa.

Akizungumza katika uwapisho wa majaji wateule jijini Dar es Salaam siku ya Jana amesema jinsi dunia inavyobadilika kiuchumi na kisiasa ndivyo Tanzania inapaswa kubadilika, na mabadiliko hayo hayalengi nguzo moja ya Serikali pekee bali mahakama na bunge pia.

“Ni imani yetu kuwa mlioteuliwa mtakwenda kufanya kazi kwa jitihada zenu zote katika Mahakama Kuu ili yale tunayoyatarajia yaonekane, mabadiliko tunayoyazungumza basi tuyaone ndani ya mahakama”.

“Wakati Serikali inajitahidi kuimarisha mahakama na watendaji ndani ya mahakama tunaomba muongeze nguvu ili mwende mfanye vizuri,” amesema.

Aidha, amesema madhumuni ya Serikali ni kuimarisha mahakama ili kuondoa mlundikano wa kesi na kuongeza ufanisi mahakamani, na moja ya hatua ambayo Serikali imechukua ni kuongeza idadi ya majaji ili kusaidia kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya