Umoja wa wanazuoni wa kiislamu Hayatul Ulamaa umeandaa kongamano la kimalezi kwa wanawake na wanaume lililopewa jina la ‘Reforming Generation’.
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere siku ya jumamosi ya tarehe 12 Agosti, 2023.
Mashekh mbalimbali wa kimataifa watakuwepo akiwepo Sheikh Abu Taymiyyah kutoka Uingereza, Sheikh Said Rageah kutoka Canada, Sheikh Jamaldeen Osman kutoka Kenya pamoja na Sheikh Shams Elmi.
Kongamano hili ni makhususi kwa jamii ya kiislamu katika kuhakikisha linaboresha maadili na kuishi kwa kufuata misingi ya dini katika zama hizi zenye changamoto nyingi.
Aidha tiketi zinapatikana kwa gharama ya shilingi Elfu kumi tu kwa kila mtu mmoja, tiketi zinapatikana katika vituo mbalimbali kama vile kanzu point, Ibn Hazm Mtambani na kariakoo, Gongo la Mboto msikiti wa Ijumaa, Tandika Masjid Irshad Chihota pamoja na Mbagala rangi tatu.