ZINAZOVUMA:

“Tuache kuchezea imani”

Msanii Steve Nyerere atamani kuingia kwenye uislamu baada ya kuona...

Share na:

Ndio anasema inatosha watu waache kuchezea imani.

Msanii Steve Nyerere amejitokeza na kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kufuatia matendo ambayo yeye anasema ni kuichezea imani.

Hii imekuja mara baada ya mhubiri kutoka mwanza anaefahamika kama “Mfalme Zumaridi” kueleza kuwa yeye alikutana na Mungu akiwa darasa la tatu.

Maneno yake hayo yalipokelewa kwa hisia tofauti huku baadhi ya watu wakifanya dhihaka mitandaoni kupitia maneno hayo..

Jambo hilo limemfanya msanii Steve Nyerere kutamani kuingia kwenye uislamu kwani usilamu hauna utani katika Mambo yanayohusu imani Yao.

Haya ndio aliyoandika msanii huyo…

“Ifike mahara tuheshimu dini zetu, matamko kama haya yana athari kubwa sana kwenye jamii, tunaweza kuona leo ni vichekesho lakini kadri siku zinavyokwenda kizazi chetu ambacho ni kizazi cha kuombewa sana nadhani nadhani kitaathirika na hizi kauli.

Najiuliza why kila mtu anataka kuwa Pastor? ni kweli ukijua kuongea sana unaona unaweza kuwa Pastor?
Siku hadi siku wachungaji wanamiminika najiuliza hivi imekuwa ni biashara! na kama biashara wanadhani kufanya mzaha na hisia za watu wanaomtafuta Mungu kwa gharama yoyote wanawatendea haki?

Najiuliza mbona wenzetu Islamu hawana utoto huu, wanaheshimu dini yao nani anayeweza kutoka kwenye Islamu akaongea kama hivi kwanini kila siku sisi ndio tunaanda trend za kucheza na kumtania Mungu wetu?

Hili ni tatizo kubwa siyo la kufumbiwa macho

Wenzetu Kenya wameanza kufungia wachungaji feki wapotoshaji, mpaka upale leseni ndio unaweza kuendelea kutoa upako, lakini siyo upako huu wa kutrend.

Nakaa nawaza naangalia haya kuanzia kwa wenzetu mataifa makubwa kuanza kukubali ndoa ya jinsia moja.”

Hayo ndio maneno aliyozungumza Steve Nyerere.

Hii ni heshima katika uislamu kuwa dini yenye kuheshimika na misingi imara kupelekea hata wasiokuwa waislamu kulitambua hilo..

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya