ZINAZOVUMA:

Tinubu kuapishwa leo Nigeria

Gavana wa zamani wa Lagos Bola Ahmed Tinubu anatarajiwa kuapishwa...

Share na:

Gavana wa zamani wa Lagos, Bola Ahmed Tinubu,ataapishwa leo kuwa Raisi mpya wa Nigeria, hii inafuatia uchaguzi uliofanyika mwezi Februari mwaka huu huku viongozi mbalimbali wa Afrika wakihudhuria kushuhudia.

Baadhi ya Viongozi Wakuu waliowasili jijini Abuja ni pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Paul Kagame (Rwanda), Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini), Abdelmadjid Tebboune (Algeria) na Denis Sassou Nguesso (Jamhuri ya Congo).

Wengine ni Umaro Sissoco Embalo wa Guinea Bissau, Julius Maada Bio wa Sierra Leone, Evariste Ndayishimiye wa Rwanda, Mahamat Deby Raisi wa Mpito wa Chad, Mohamed Bazoum wa Niger, Nana Akufo-Ado wa Ghana na Musalia Mudavadi atakayemwakilisha Rais William Ruto wa Kenya.

Bola Tinubu, Gavana wa zamani wa Lagos na Mwanachama wa Chama Tawala (APC), anatarajiwa kuapishwa leo Mei 29, 2023 kuwa Rais wa 16 wa Nigeria baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika Februari 25, 2023.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya