ZINAZOVUMA:

Tanzia: Membe amefariki

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani Benard...

Share na:

Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani na aliyewahi kuwa mgombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo mwaka 2020, Bernard Membe, amefariki dunia.

Benard Membe amefariki akiwa katika Hospitali ya Kairuki, Jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kifua kwa muda mfupi.

Bernard Membe alihudumu katika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Mwaka 2007 hadi 2015.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameelezea kusikitishwa kwake na kifo cha Benard Membe akitoa pole na salamu za rambirambi kwa familia na watanzania.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya