ZINAZOVUMA:

Tanzania yapiga hatua kusimamia ustawi wa rasilimali watu

Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amesema Tanzania imeimarisha sekta...

Share na:

Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kusimamia ustawi wa Rasilimali watu kwa kuimarisha sekta mbalimbali nchini zikiwemo sekta za elimu, afya na tehama.

Mbali na sekta hizo, maeneo mengine ni uimarishaji wa sekta binafsi na sekta nyingine muhimu zinazochagiza ustawi wa rasilimali watu.

Dkt Mpango ameyasema hayo leo Julai 25, 2023 wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa Wakuu wa nchi za Afrika kuhusu ‘Rasilimali Watu’ katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema Tanzania imefanikiwa kupiga hatua hizo sababu ya uboreshwaji wa miundombinu ya elimu, utoaji wa elimu bure, kuruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo.

Hatua nyingine ni pamoja na uimarishaji wa sekta ya afya, ikiwemo manunuzi ya mashine ya MRI, CT- Scan na kuboresha sekta ya mawasiliano.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya