ZINAZOVUMA:

Tanzania yaipa msaada uturuki.

Serikali ya Tanzania imetoa msaada wa kibinadamu kwa uturuki kufuatia...

Share na:

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi msaada wa kibinadamu kwa Serikali ya Jamhuri ya Uturuki kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo tarehe 6/02/2023 na kusababisha madhara makubwa kwenye miji ya Kusini Mashariki mwa Uturuki .

Mheshimiwa Lt Jen (Mst) Yacoub Hassan Mohammed, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki alikabidhi msaada huo kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Bw. Muhammet Maruf Yaman, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Taasisi inayohusika na majanga (AFAD) alipokea kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Uturuki.

Mheshimiwa Balozi Jenerali Mohamed alitumia fursa hiyo kuwasilisha pia salamu za pole kutoka kwa Mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Watanzania kwa ujumla kwenda kwa Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki na Raia wa Uturuki kufuatia madhara yaliyosababishwa na tetemeko hilo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya