ZINAZOVUMA:

Tanzania kulipa TZS bilioni 266

Kituo cha kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji kimeiamuru...

Share na:

Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 sawa na TZS bilioni 266 kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi uliochukuliwa wakati wa utawala wa Hayati Rais Dkt. John Magufuli mwaka 2018 wa kufuta leseni yao ya uchimbaji wa madini ya nikeli.

Kampuni hizo zilifungua kesi na kufanikiwa kuishinda Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka wajibu wake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Pamoja (BIT) kati ya Uingereza na Tanzania na sheria za kimataifa kwa kutaifisha leseni hiyo..

Tanzania pia imeamriwa kulipa dola milioni 3.859 sawa na TZS bilioni 9.3]kama gharama za kisheria kwa walalamikaji, pamoja na ada na gharama za ICSID.

Kampuni ya Australia, Indiana Resources Ltd ambayo ni mmiliki mkuu wa mradi wa nikeli wa Ntaka, hapo awali ilionya kuwa itachukua ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL). Indiana sasa inasema itachukua hatua haraka kutekeleza uamuzi wa mahakama.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya