ZINAZOVUMA:

Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa AFCON 2027.

Nchi ya Tanzania, Kenya na Uganda zimeungana pamoja kuomba kuwa...

Share na:

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepokea maombi kutoka kwa nchi sita kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 ikiwemo Tanzania.

Baada ya kufika muda wa mwisho kupokea maombi uliowekwa na CAF, jumla ya waombaji sita walifanikiwa kuwasilisha maombi yao.

Kwa mujibu wa CAF, nchi zilizowasilisha maombi hayo ni Algeria, Botswana na Misri.

Wakati Kenya, Uganda na Tanzania zimewasilisha maombi ya kuandaa fainali hizo kwa pamoja.

Hatua inayofuata ni kuwasilisha zabuni ya mwisho ifikapo Mei 23, 2023 ikijumuisha nyaraka zote (makubaliano ya uenyeji, makubaliano ya miji mwenyeji, dhamana ya serikali, na nyinginezo).

Ukaguzi utaanza kufanyika Juni 1-15, 2023 na uamuzi wa nani atakuwa mwenyeji wa fainali hizo utafanywa na Kamati ya Utendaji ya CAF.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya