ZINAZOVUMA:

Tanzania, China na Uholanzi kuendeleza ushirikiano worldveg

Katibu Mkuu wizara ya kilimo awasisitiza watafiti wa mbogamboga worldveg...

Share na:

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema Serikali za Tanzania, China na Uholanzi zitaendelea kushirikiana kukiendeleza Kituo cha Taasisi ya Utafiti na Uendelezaji wa Mazao ya Mbogamboga Duniani cha World Vegetable Centre (worldveg) ili kukidhi mahitaji ya wakulima.

Mweli alisema hayo wakati akizindua Benki ya Afrika ya vinasaba vya mbegu za mboga za asili katika kituo cha Worldveg kilichopo Tengeru mkoani Arusha. Ndugu Mweli amewataka watafiti kutimiza majukumu yao kikamilifu ili benki hiyo isiwe ya makumbusho kwani uhifadhi wa mbegu unapaswa kuwasaidia wakulima wa Afrika.

Alisema hadi sasa benki hiyo inahifadhi zaidi ya aina 5,000 ya mbegu za mboga mboga, na ilitegemewa hadi kufikia 2025/26 iwe na aina 15,000 ya mbegu zimehifadhiwa katika benki hiyo. Hii ni kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa afrika kuwa na mbegu za asili Afrika na duniani.

Aliendelea kusema kuwa msingi wa kituo hicho ni kwa ajili ya wakulima duniani na sio Afrika pekee yake, hivyo basi jitihada za ziada zinahitajika kwa wataalamu wa utafiti kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili mbegu za asili za mboga ziweze kuwasaidia wakulima mashambani.

Na kuongeza kuwa mbegu za asili za mbogamboga zinapaswa kutunzwa katika benki hiyo ya pili duniani ili kizazi kijacho kiweze kujua historia ya mbegu hiyo. Na watafiti hao wanapaswa kufanya utafiti wa sasa na utafiti wa kizazi kijacho kwa maslahi ya wakulima.

‘’Tuhifadhi mbegu kwa ajili ya tafiti bora kwa ajili ya wakulima na tusihifadhi mbegu kwa ajili ya maonyesho ya makumbusho hilo haliwezekani’’alisema Mweli

Katibu Mkuu Mweli alisema serikali itatoa eneo lingine kwa ajili ya Worldveg kwani eneo walilonalo la ekari 14 haitoshi kwani limejaa kwa ajili ya matumizi ya tafiti na bustani za mafunzo za mbogamboga.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Worldveg Afrika, Gabriel Rugalema aliwashukuru wafadhili wote waliofanikisha ujenzi na uletaji wa vifaa vya kisasa katika Benki ya Vinasaba vya mbegu na kusema kuwa taasisi hiyo haitawaangusha kwani watafanya kazi kwa kujituma kwa ajili ya wakulima na kuinua uchumi wa wakulima Afrika.

Rugalema alisema Benki ya Vinasaba vya mbegu Afrika ni benki pekee Afrika hivyo ni sifa kwa Tanzania na Afrika na watatumia nafasi hiyo kutunza,kukuza na kuendeleza mbegu za asili za mboga mboga kwa maslahi ya wakulima.

Pia amewataka wanasayansi kutumia nafasi ya uwepo wa Benki ya Vinasaba ya mbegu Afrika katika tafiti mbalimbali lengo likiwa moja la kutaka wakulima kuwa na mbegu bora yenye kuwanufaisha katika mazingira tofauti ya ukame na mabadiliko ya tabia nchi.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya