Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa uwanja wa Taifa una hudumiwa na vyanzo viwili vya Umeme. TANESCO na Majenereta ya uwanja.
Taarifa hiyo imekuja baada ya kutokea hitilafu ya taa za uwanjani kuzimika katika mchezo wa Yanga dhidi ya Rivers siku ya jana tarehe 30 Aprili.
TANESCO wamesema mechi ya jana umeme uliokuwa ukitumika haukua wa Tanesco bali ulkua wa majenereta ya uwanjani kama ambavyo taratibu za CAF zinaelekeza.
Baada Majenereta kushindwa kufanya kazi katikati ya mchezo na taa kuzimika uwanja uliamua kutumia chanzo cha TANESCO na mchezo ukaendelea.
TANESCO wameahidi kushirikiana ili kudhibiti kadhia hiyo wakati mwingine.
“Tunasikitika kwa kadhia iliyo iliyo jitokeza na tutashirikiana na wenzetu kwa siku za usoni jambo hili lisijirudie.”