ZINAZOVUMA:

Taasisi ya JKCI yaja na suluhisho ukosefu wa nguvu za kiume

Taasisi ya JKCI inatarajia kuanza tiba ya kuzibua mishipa ya...

Share na:

Katika kukua kwa teknolojia ya matibabu, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kuanza kutoa tiba ya kuzibua mishipa ya uume katika kukabiliana na upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wanaokabiliwa na shida hiyo.

JKCI imefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza mdogo wa moyo wa kuzibua mishipa ya damu ya miguuni iliyoziba na huduma hiyo kwa wanaume wenye changamoto ya nguvu za kiume inatarajiwa kuanza kutolewa baadaye Oktoba mwaka huu.

“Oktoba tutaanza kutoa huduma mpya tukishirikiana na wenzetu wa India, tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume ni kubwa na linazidi kuongezeka kutokana na mishipa ya uume kuziba na hivyo mwanaume anashindwa kuhimili,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dkt Peter Kisenge.

Dkt Kisenge amesema tatizo hilo ni kubwa japo hakuna utafiti walioufanya, lakini wapo wanaume wenye tatizo hilo wanafika JKCI wakihitaji huduma.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya