Timu za Simba na Yanga zimefanikiwa kutinga katika hatua za robo fainali katika michuano ya kimataifa.
Simba ikitinga hatua hiyo katika mashindano ya klabu Bingwa Afrika huku Yanga wao ni katika mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Ni rekodi mpya ambayo inewekwa baada ya timu zote mbili za Tanzania kutinga katika hatua hiyo, Simba ikiifunga Horoya magoli 7 kwa bila huku Yanga akimfunga nwarabu wa Tunisia Us monastry.
Hii ni hatua kubwa kama Taifa na rekodi ya kwanza katika historia ya mpira nchini Tanzani kufanikiwa kuingiza timu mbili katika hatua ya robo fainal.
Lakini pia hii ni rekodi kwa timu ya Yanga kwa kuingia katika hatua hiyo kwa mara ya kwanza huku wakiwa wanaongoza kundi kwa tofauti ya magoli na timu inayoshika nafasi ya pili.
Wadau mbalimbali wamepongeza hatua kubwa zinazopigwa na timu hizi huku wengi wakisifia uwekezaji unaofanywa na klabu hizi hasa katika usajili wa wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuleta matokeo hasa katika mechi ngumu.
Kwa Yanga imeonesha mwanga kuwa nao hivi sasa wamewekeza vya kutosha na kufanya vizuri katika mashindano haya kama ambavyo Simba amekua akifanya na kufanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali mara kadhaa katika mashindano ya kimataifa.
Haya ni maendeleo katika mpira wetu tunaweza sema sasa mpira wa Tanzania unakua na hii ni kutokana na hamasa inayotolewa na viongozi wa timu hizi lakini pia ikiwemo hamasa inayotolewa na serikali kupitia goli la mama.