ZINAZOVUMA:

Sierra Leone: wachimba makaburi kutengeneza dawa za kulevya

Watengeneza madawa waanza kuchimba makaburi li kupata mifupa kama kiambato...

Share na:

Waraibu wa dawa za kulevya nchini Sierra Leone, wanachimba makaburi ili kupata malighafi ya kutengeneza madawa za kulevya ziitwazo ‘Zombie’.

Dawa hizo za kulevya hutumia mifupa ya binadamu iliyoharibika kiasi, hali iliyosababsha watengenezaji kufukua makaburi ili kupata malighafi (mifupa).

Mamlaka nchini humo kwa sasa inalinda makaburi ili kuzuia uhalifu huo wa kuchimba wa mifupa kwa ajili ya utengenezaji wa dawa za ‘Zombie’.

Dawa hiyo, pia inafahamika kama ‘kush’, ina mfupa wa binadamu uliosagwa kama mojawapo ya viambato vyake kuu.

Dawa hiyo ya mihadarati ilionekana kwa mara ya kwanza nchini Sierra Leone mwaka wa 2018.

Matumizi mabaya ya mihadarati imeongezeka na kuwa changamoto ambayo haijawahi kushuhudiwa kwenye serikali ya mitaa.

Wafanyabiashara sasa wanageuka kuwa wezi wa makaburini, kuvunja maelfu ya makaburi ili kuiba mifupa ili kuendana na mahitaji yao.

“Nchi yetu kwa sasa inakabiliwa na tishio lililopo kutokana utumiaji na athari mbaya za dawa za kulevya, haswa dawa mbaya ya sintetiki Kush,” Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio alisema, kulingana na BBC.

Bio, pamoja na kukiri “kuongezeka kwa vifo” kati ya watumiaji wa dawa za kulevya, pia alisema kuwa ameunda kikosi kazi cha kutokomeza tishio la dawa za kulevya nchini humo.

Sierra Leone sasa inajenga vituo katika kila wilaya “vina wahudumu wa kutosha na wataalamu waliofunzwa kutoa huduma na usaidizi kwa watu walio na uraibu wa dawa hizo”.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya