ZINAZOVUMA:

Shule ya msingi mwisho darasa la sita

Taasisi ya Elimu Tanzania imetoa mtaala mpya wa elimu ambapo...

Share na:

Taasisi ya Elimu Tanzania imetoa mtaala wa elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba 2023.

Muundo wa mtaala huo umebadilika na sasa elimu hiyo itakuwa ni ya miaka sita badala ya saba kama ulivyokuwa Mtaala wa Elimu ya Msingi wa mwaka 2016.

Mtaala huo umezingatia nadharia za ukuaji na ujifunzaji na falsafa ya elimu ya kujitegemea inayosisitiza elimu inayomwezesha Mtanzania ajitegemee na amudu maisha yake ya kila siku.

Muundo wa mtaala unaonesha elimu ya msingi itatolewa kwa miaka sita katika hatua mbili ambazo ni darasa la kwanza na la pili ili kujenga umahiri katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Katika hatua ya pili inaonesha mtaala huo utaanzia darasa la tatu hadi la sita na italenga kuimarisha stadi za KKK na stadi nyingine za maisha.

Mwanafunzi wa shule ya msingi anatakiwa aanze darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka sita na kumaliza darasa la sita akiwa na umri wa miaka 11.

Kwa mujibu wa mtaala huo, maeneo ya kujifunza na umahiri mkuu kwa darasa la kwanza na la pili yamezingatia ujenzi wa lugha, mawasiliano na stadi za hisabati, utamaduni, sanaa, michezo na afya na mazingira.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,