ZINAZOVUMA:

Serikali yaongeza nguvu kupambana na Malaria.

Serikali imeendelea kutoa kipaumbele katika kutokomeza ugonjwa wa Malaria unaoendelea...

Share na:

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa leo Aprili 25, 2023 amemuwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassani katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria duniani kwa Mwaka 2023 ambapo Kitaifa yanafanyika Jijini Dar es Salaam.

Katika maadhimisho hayo Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kutoa kipaumbele kikubwa katika kutokomeza ugonjwa wa Malaria kwa kuwa ugonjwa huu bado ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha athari nyingi kwa Watanzania ikiwemo vifo hapa nchini.

Na kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nauye amevitaka vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na makampuni ya simu kuhakikisha vinakuwa na mipango endelevu ya kuifanya Tanzania inakuwa na 0 ‘Zero’ Malaria na kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake.

Kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya Malaria mwaka 2023 ni “Wakati wa Kutokomeza Malaria ni Sasa: Badilika, Wekeza, Tekeleza – Ziro Malaria Inaanza na Mimi”.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya