ZINAZOVUMA:

Serikali kuanzisha kanzi data Kwa makundi maalumu ya damu.

Serikali kupitia wizara ya Afya imedhamiria kuanzisha kanzi data ya...

Share na:

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Serikali inadhamiria kuanzisha kanzi data ya kutambua makundi ya damu kwa Watanzania wote, ili kusaidia kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa damu salama kwa watu wenye makundi adimu ya damu.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mpango wa taifa wa damu salama kwa waziri wa afya Ummy Mwalimu kwamba inayo kanzi data ya watu takribani 350 ambao wapo kwenye kundi O-Negative baada ya kuwatambua kama Kundi adimu la damu.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo Aprili 11, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara katika Ofisi za mpango wa Taifa wa damu salama ili kukagua na kuangalia hali ya upatikanaji wa damu hapa nchini.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,