ZINAZOVUMA:

Samia: kumbadilisha kijana wakiume si rahisi.

Raisi wa Samia amesema ni rahisi kumbadilisha binti wa kike...

Share na:

Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassani ameshiriki katika Baraza la Eid El Fitr lilofanyika siku ya Jana tarehe 22 Aprili 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam.

Raisi Samia wakati akizungumza katika Baraza hilo alisema ni rahisi kumbadilisha mtoto wa kike anapopotea lakini si rahisi kwa mtoto wa kiume hivyo kuwataka wazazi kuwa makini katika suala zima la malezi kwa vijana.

“Wazazi wakiacha asili na kufanya watoto wasikue kulingana na asili zetu, tutatengeneza watoto ambao watabadilishwa akili na kufuata mwelekeo mwingine”.

Baraza la Eid lilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa dini wakiongoza na Muft na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Bin Zubeir Bin Ally pamoja na waumini wa kiislamu.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya