ZINAZOVUMA:

Sababu ya kushuka thamani kwa sarafu za EAC

Uzalishaji mdogo na utegemezi wa bidhaa kutoka nje ndio sababu...

Share na:

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), John Kalisa amesema uzalishaji mdogo na utegemezi mkubwa wa bidhaa kutoka nje ndio unaosababisha kushuka kwa thamani ya sarafu za nchi za Afrika Mashariki.

“Usafirishaji wetu nje ya nchi ni mdogo kuliko uagizaji. Hili limeweka shinikizo kubwa kwa thamani ya sarafu zetu,”

Amesema ili kukabiliana na kuporomoka kwa sarafu, nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), hazina budi kuongeza tija na thamani ya mauzo ya nje.

Kalisa amesema sababu nyingine za kushuka kwa sarafu za EAC dhidi ya sarafu za kigeni ni kuongezeka kwa deni la mataifa hayo kutokana na miradi mikubwa inayotekelezwa.

Ripoti ya hivi karibuni ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ilionyesha nchi ya Kenya ambayo ndiyo kubwa kwa uchumi (EAC), ilishuhudia kushuka kwa sarafu yake kwa kiwango kikubwa kuliko nchi nyingine ndani ya jumuiya hiyo.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya