ZINAZOVUMA:

Rwanda yasikitishwa na kitendo cha Ubelgiji

Msemaji wa serikali ya Rwanda amesema kwamba uamuzi uliofanywa na...

Share na:

Serikali ya Rwanda imetoa malalamiko kwa baada ya kukataliwa kwa Balozi Vincent Karega alieteuliwa kuwa balozi nchini Ubelgiji.

Rwanda imesema kwamba uamuzi huo uliofanywa na Ubelgiji sio mzuri kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo alinukuliwa akisema “Inasikitisha kuona kwamba serikali ya Ubelgiji inaonekana imekubali shinikizo la serikali ya DRC na ‘propaganda’ ya makundi ya waasi, ambao pia waliamua kutangaza uamuzi huo mapema”.

Katika ujumbe wake wa barua pepe, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ubelgiji, Nicolas Fierens Gevaert alisema kwamba nchi yake itazungumza kuhusu jambo hilo kupitia njia za kidiplomasia.

Alisema: “Ubelgiji itatoa taarifa kupitia njia za kidiplomasia. Masuala hayo yatashughulikiwa kupitia njia za utawala. Tunatumai kuwa na uhusiano mzuri na wa amani wenye kujenga baina yetu na Rwanda.”

Karega, mwenye umri wa miaka 60, alitarajiwa kuchukua nafasi ya balozi Dieudonné Sebashongore, ambaye aliiwakilisha Rwanda nchini Ubelgiji tangu 2020.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,