ZINAZOVUMA:

Rwanda imekanusha kuhusishwa na waasi wa Burundi

Share na:

Serikali ya Rwanda imekanusha tuhuma ya Burundi kwamba, ilikipatia silaha kikundi cha waasi kilichoshutumiwa juu ya mlipoku wa guruneti jijini Bujumbura.

Shambulio hilo lililotokea siku ya ijumaa katika jiji la Bujumbura na kusababisha majeruhi kadhaa, limezidi kuufanya uhusiano wa mataifa hayo mawili wanachama wa Afrika Mashariki kuwa mbaya.

Takriban watu 38 walijeruhiwa katika shambulio hilo, na wizara ya mambo ya ndani ya Burundi ilisema, kuwa wanaamini waasi wa RED-Tabar ndio wamefanya shambulizi hilo.

Burundi ilitangaza kuwa, Rwanda ilitoa mafunzo na msaada wa silaha kwa waasi hao, ambao wamekuwa wakipigana na serikali ya Burundi kutoka katika kambi zao zilizopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo alikanusha madai hayo, na kusema kuwa serikali ya Rwanda haina uhusiano wowote na shambulio hilo.

“Burundi ina tatizo na Rwanda, ila sisi Rwanda hatuna tatizo na Burundi” iliendelea kusema taarifa ya kutoka ofisi hiyo ya Msemaji.

Tunatoa wito kwa Burundi kutatua matatizo yake ya ndani na kutoihusisha Rwanda na mambo hayo mabaya.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya