Raisi wa Kenya na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama nchini humo Dkt. William Ruto, amemteuwa na kumuapisha Luteni jenerali Charles Muriu Kahariri kuwa mkuu wa Majeshi mpya wa majeshi ya ulinzi na usalama (CDF).
Luteni jenerali Charles Muriu alikuwa Mkuu wa Jeshi la Wanamaji na Naibu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Kenya (VCDF), ameapishwa na kuchukua nafasi ya jenerali Francis Omondi Ogolla aliyefariki dunia kwa ajali ya Helikopta iliyotokea Jana April 18, 2024.
Luteni jenerali Kahariri sasa ana wajibu wa kuongoza maziko ya jenerali Francis Omondi Ogola yatakayofanyika Aprili 21, 2024 katika kaunti ya Saiya nchini humo.