ZINAZOVUMA:

Ruto amtuhumu Kenyatta kufadhili maandamano

Raisi wa Kenya William Ruto anamtuhumu Raisi aliyepita Uhuru Kenyatta...

Share na:

Rais wa Kenya, William Ruto amemtuhumu mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta kuwa anafadhili maandamano ya upinzani nchini humo.

Akizungumza huko Kaunti ya Nakuru jana Julai 14, 2023, Ruto amedai kuwa Kenyatta alikuwa akiwafadhili vijana wa Mungiki kufanya fujo wakati wa maandamano ya Azimio la Umoja nchini humo.

Rais Ruto ameonya kuwa ikiwa Rais huyo wa zamani ataendelea kufadhili shughuli za Azimio, atalazimika kumchukulia hatua.

Amemtaka Kenyatta kuwa muungwana, akisema kuwa yeye alimuunga mkono katika kipindi akiongoza nchi hiyo, huku akimtaka Kenyatta kuacha kujihusisha na kiongozi wa ODM, Raila Odinga.

“Nikuombe rafiki yangu Uhuru, achana na huyo mzee (Raila), acha kutoa pesa za kuajiri mungiki kuiharibu Nairobi, wewe ulikuwa Rais tukakuunga mkono, tafadhali kuwa muungwana,” amesema Rais Ruto.


Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya