Rais wa Kenya, William Ruto ameondoa marufuku ya ukataji miti iliyokuwa imewekwa nchini humo kwa miaka sita iliyopita akisema marufuku hiyo iliathiri watu wengi waliokuwa wakitegemea mbao kama chanzo cha mapato.
Ruto ametoa kauli hiyo jana Jumapili Julai 2, 2023 mjini Molo ambapo amesema kuwa kuna haja ya kubuni nafasi za kazi na kufungua sekta za uchumi zinazotegemea mazao ya misitu.
Kuondolewa kwa marufuku hiyo kunakuja wakati Serikali ya Kenya ikiendelea na mpango wake wa kupanda miti bilioni 15 katika kipindi cha miaka 10 ili iweze kuongezeka nchini humo.
Mwaka 2018 Serikali ya Kenya ilipiga marufuku ukataji miti kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.