ZINAZOVUMA:

Raisi Samia asema hatoruhusu mtu yoyote kuligawa Taifa hili.

Raisi Samia amewataka Watanzania kutoruhusu watu au kikundi cha watu...

Share na:

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Watanzania kuwaenzi Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kulinda Uhuru wa Tanzania kwa kudumisha amani, umoja, mshikamano na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania.

Amesema hayo leo wakati akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika katika Mji wa Serikali, Mtumba katika Uwanja mpya wa Mashujaa, mkoani Dodoma.

Aidha, Rais Samia amewahimiza Watanzania kutowaruhusu watu au kikundi cha watu wenye nia ovu ya kutaka kuligawa taifa kwa kisingizio chochote kile kwani Tanzania ni moja na haiwezi kugawanyika.

Mbali na hayo, ameielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na wahusika wote kuendelea kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa mnara na uwanja wa Mashujaa ili ukamilike kwa wakati na kwa viwango kama ilivyokusudiwa. Vile vile ameitaka Wizara ya Fedha ihakikishe inatoa fedha kwa kuzingatia mpango kazi wa ujenzi bila kuwepo kwa ucheleweshwaji.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya