ZINAZOVUMA:

Rais William Ruto Aapa Kukabiliana na Maandamano ya Upinzani

Rais William Ruto wa Kenya amejibu tangazo la kiongozi wa...

Share na:

Raisi wa Kenya William Ruto ameapa kuwa maandamano dhidi ya serikali ya siku tatu mfululizo yaliyotangazwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuanzia wiki ijayo, kuwa hayatafanyika.

Hata hivyo pia Raisi Ruto amemuonya kiongozi huyo wa Muungano wa Azimio Raila Odinga na kuahidi kuwa atakabiliana naye.

“Uchaguzi umekwisha. Huwezi kutafuta uongozi kwa kutumia damu za Wakenya na kuharibu mali zao,” amesema hayo akiwa mjini Naivasha.

“Damu hizi hazitatokea, Nisikilize kwa makini Huwezi kutumia njia zisizo za kisheria, zisizo za kikatiba kutafuta mamlaka nchini Kenya, subiri 2027. Nitakushinda tena.”

Awali, kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, alitangaza kuwa maandamano dhidi ya serikali yatafanyika kwa siku tatu mfululizo wiki ijayo kuanzia Jumatano hadi Ijumaa.

Muungano huo ulisema hatua hiyo imetokana na matakwa ya umma, na kupitia tena mpango wake wa awali ambao ulikuwa umesema kuwa maandamano, yatafanyika siku ya Jumatano pekee.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya