ZINAZOVUMA:

Rais wa zamani wa Zambia aishtaki serikali kumzuia kusafiri

Raisi wa zamani wa Zambia Edgar Lungu ameishtaki serikali ya...

Share na:

Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu, ameipeleka Serikali ya nchi hiyo mahakamani baada ya kudai kuzuiwa kusafiri kwenda Korea Kusini kwenye mkutano.

Inadaiwa kuwa Lungu alialikwa kwenye mkutano wa amani duniani nchini Korea Kusini lakini alipokaribia kuondoka alishushwa kwenye ndege yake kwa sababu hakuwa na kibali cha serikali cha kusafiri.

Edgar Lungu sasa anatafuta mapitio ya mahakama katika Mahakama Kuu ya Lusaka, kwa mujibu wa nyaraka alizowasilisha mahakamani, anapinga uamuzi wa Serikali kumzuia kusafiri kwenda Korea Kusini.

Chama chake cha Patriotic Front (PF), kimelaani kitendo hicho kinachodaiwa kufanywa na Serikali, kikitaja kuwa ni kinyume cha sheria.

“Ikiwa amealikwa na safari, atalipiwa au anaweza kukidhi gharama za safari yake mwenyewe na ya wapambe wake, hahitaji kuijulisha Serikali,” amesema Emmanuel Mwamba, msemaji wa PF.

Mwamba amesema Rais huyo wa zamani, awali alizuiwa kusafiri kwa matibabu licha ya kuomba kibali kutoka katika ofisi ya Baraza la Mawaziri.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya