ZINAZOVUMA:

Rais Samia Ahimiza wananchi kulipa Kodi

Katika Baraza la Idd el Fitr Rais samia awakemea wafanyabiashara...

Share na:

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuendelea kulipa kodi ili serikali ikusanye mapato kwa haki yatakayoiwezesha kutimiza wajibu wake ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kijamii

Rais Samia ametoa wito huo kwenye Baraza la Idd el- Fitri lililofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

Pia amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa mbinu mbalimbali ikiwemo kutokutoa risiti au kutoa risiti za kiasi pungufu na kwa wanunuzi wa bidhaa kutokudai risiti.

Rais Samia amesema serikali inaweza kuimarisha zaidi huduma za jamii ikiwa itafanikiwa kukusanya zaidi na kupunguza ukwepaji wa kodi kwa kuzingatia idadi ya Watanzania na kiwango cha biashara zinazofanyika nchini.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,