Jeshi la Polisi mkoani Manyara linawashikilia raia 17 wa Ethiopia ambao wanaodaiwa kuingia nchini bila kibali. Waethiopia hao walikuwa njiani wakielekea Afrika Kusini kupitia mkoani Dodoma.
Akizungumza katika Operesheni hiyo Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Manyara Lucas Mwakatundu amesema waethiopia hao wamekamatwa April 7 mwaka huu katika mtaa wa Maisaka mjini Babati.
Na kuongeza kuwa walikuwa na gari yao binafsi ambayo imeng’olewa siti ili waenee.
Kamanda huyo amesema wamewakamata raia hao wa ethiopia wakiwa na gari yenye namba za usajili zaidi ya moja.
Namba za usajili za gari hiyo ni za Tanzania na moja ni ya serikali STL1964 na namba nyingine ni T723BSF.
Bado haijajulikana mmiliki wa gari hiyo aina ya Land Cruiser V8 VXR, na polisi watawakabidi kwa Idara Uhamiaji kwa hatua nyingine zaidi ikiwemo kuwafikisha mahakamani kwa mashata yao.