ZINAZOVUMA:

Raia 10 wa Congo wauawa Sudan

Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema raia wake...

Share na:

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema raia wake 10 wamefariki baada ya chuo chao walichokua wanasoma kushambuliwa katika mashambulizi ya anga katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum siku ya Jumapili.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema katika taarifa yake kwamba imepokea kwa masikitiko makubwa mauaji ya raia wake katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika.

Waziri Christophe Lutundula alisema kuna dalili kwamba mashambulizi hayo ya anga yalifanywa na jeshi kwenye eneo wanapoishi raia na watu wasio na silaha, wakiwemo raia wa kigeni na kupelekea kuwajeruhi vibaya raia hao.

Waziri huyo amesema serikali inasubiri mamlaka ya Sudan kutoa mwanga zaidi kuhusu tukio hilo.

Khartoum imekumbwa na mapigano kati ya jeshi na wapinzani wao wa kijeshi (RSF) tangu Aprili 15, huku raia wakinaswa katika mapigano hayo.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya