Rais wa Urusi Vladimir Putin hatahudhuria mkutano wa viongozi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya BRICS ana kwa ana, badala yake atahudhuria kwa njia ya mtandao.
Hayo yameandikwa na mtandao wa Time kuwa; “wakati viongozi wengine wa mataifa ya BRICS watahudhuria mkutano huo, huku wengine wakiwasili jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Rais Putin atashiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao (video conference)”.
Sababu ya kufanya hivyo inaelezwa ni kutokana na hati ya kukamatwa kwa Rais huyo, iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC); ambayo kimsingi iliiweka Afrika Kusini (mwenyeji), kwenye wakati mgumu, hatimaye kusababisha Putin kubaki nyumbani.
Mkutano huo wa siku tatu umeanza jana Jummane Agosti 22, 2023 katika jiji kubwa na kitovu cha kifedha nchini Afrika Kusini.