ZINAZOVUMA:

PSG yaruhusu Al-Hilal kuzungumza na Mbappe

Klabu ya Paris Saint Germain PSG imeiruhusu klabu ya Al-Hilal...

Share na:

Klabu ya PSG imeipa ruhusa klabu ya Al-Hilal ya nchini Saudi Arabia kufanya mazungumzo na nyota wao Kylian Mbappe baada ya kuwa wametangaza dau la £300 milioni ili kumpata mchezaji huyo.

Mbappe ana mkataba na timu yake ya PSG mpaka mwaka 2024 lakini ameiambia klabu yake hiyo kuwa hatosaini mkataba mwingine kuendelea kuitumikia PSG.

Hata hivyo kumekua na mgogoro baina ya mchezaji na klabu, baada ya PSG kugundua kuwa Mbappe amefanya mazungumzo na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

Ikiwa PSG hawatomuuza nyota huyo wa Ufaransa basi msimu ujao ataondoka akiwa mchezaji huru jambo ambalo PSG kwao litakua ni hasara.

Vyanzo vya mchezaji huyo vinasema kwamba bado mchezaji huyo anataka kuendelea kucheza barani Ulaya na si vinginevyo.

Ikiwa kama ofa ya Al-Hilal itafanikiwa basi ndio utakuwa usajili wa gharama zaidi kuwahi kufanyika katika historia ya mpira wa miguu.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya