ZINAZOVUMA:

Niger yaishutumu Ufaransa kuvuruga amani

Jeshi la Niger limesema Ufaransa ilikiuka zuio la anga lililotolewa...

Share na:

Jeshi la Niger linaishutumu Ufaransa kwa kuhatarisha usalama wa nchi hiyo na raia wake.

Katika taarifa yake jeshi la Niger limeishutumu Ufaransa kwa kuingia katika Anga yake ambayo Niger ilitangaza kuifunga lakini pia kuwaachia magaidi waliokuwa wanashikiliwa na jeshi la Ufaransa lililopo nchini humo ili wafanye mashambulizi.

Taarifa hiyo imesema zaidi ya magaidi 16 wameachiwa upande mmoja wa Ufaransa na wamekutana kuandaa mashambulizi katika eneo la mipaka mitatu.

Niger imesema ndege ya Ufaransa iliyoingia katika anga yake iliyoifunga, ndege hiyo ilipoteza mawasiliano kwa muda wa zaidi wa masaa manne.

Hata hivyo Ufaransa imekana shutuma zote hizo dhidi yake na kusema hazina msingi na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema wanajeshi wa Ufaransa waliopo Niger ni kwa ajili ya kupambana na makundi ya kigaidi.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya