Kampuni mpya ya Elon Musk ya Neuralink imesema imepokea kibali kutoka kwa wadhibiti wa Marekani ili kupima vipandikizi vya ubongo kwa binadamu.
Neuralink imesema kibali kilitolewa Alhamisi na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani FDA kuruhusu uchunguzi wake wa kwanza wa kimatibabu kwa kibinadamu nakusisitiza kuwa ni hatua ya kwanza muhimu kwa teknolojia yake, ambayo inakusudiwa kuruhusu akili kuingiliana moja kwa moja na kompyuta.
“Tunafurahi kwamba tumepokea idhini ya FDA kuzindua uchunguzi wetu wa kliniki ya kwanza kwa binadamu,”. Neuralink imesema katika chapisho kwenye Twitter inayoendeshwa na Musk.
“Haya ni matokeo ya kazi kubwa ya timu ya Neuralink kwa ushirikiano wa karibu na FDA.”
Elon Musk amekua akitabiri tangu 2019 kwamba kampuni yake ya kifaa cha matibabu itaanza majaribio ya kibinadamu ya kipandikizo cha ubongo kutibu hali zisizoweza kubadilika kama vile kupooza na upofu.