ZINAZOVUMA:

Nape aomba radhi kwa niaba ya Membe

Waziri wa Habari Nape Nauye amesema anaomba radhi kwa wake...

Share na:

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema katika kitabu cha historia ya maisha ya Membe alichokiandika mwenyewe enzi za uhai wake huenda kuna sehemu kitawakwaza watu hivyo anaomba samahani kwa niaba ya marehemu.

Nape ameyasema hayo wakati akitoa salamu za familia katika hafla ya kitaifa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.

“Uandishi wa kitabu hiki yawezekana kulikuwa na mahala utakwazika hapa na pale, inawezekana wakati wa kukisoma kitabu si wote wakakifurahia hivyo kwa niaba ya familia niwaombe mumsamehe ili apate kupumzika kwa Amani,” amesema Waziri Nape

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya