ZINAZOVUMA:

Mwanasiasa nchini Senegal ameweka mgomo wa kutokula

Mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal ameweka mgomo wa kutokula akiwa...

Share na:

Mwanasiasa maarufu na kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko amesema kuwa ameanza mgomo wa kula akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa wiki iliyopita, huku mawakili wake wakilaani kukamatwa kwake.

Mwendesha mashtaka wa Senegal alitangaza mashtaka mapya saba dhidi ya mwanasiasa huyo ambae ni mkosoaji mkubwa wa Rais Macky Sall.

Ousmane Sonko anadai kuwa msururu wa kesi ambazo amekuwa akibambikiwa zinalenga kumuondoa kwenye uwanja wa siasa.

“Huku nikikabiliwa na chuki nyingi, uongo, dhulma, mateso, nimeamua kustahamili”, Sonko aliandika, akiwaomba wafungwa wote wa kisiasa kuungana naye katika mgomo wa kugomea chakula.

Aidha katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Dakar, mawakili wa Sonko wamesema mamlaka nchini humo haijiheshimu haki za mteja wao.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya