Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Ally Bin Zubeir amethibitisha kutokuandama kwa mwezi na hivyo kumalizia Ramadhani ya 30 siku ya kesho.
Muft amesema wameangalia mwezi sambamba na kupokea taarifa kutoka kwa nchi za jirani kama Kenya na kwingineko ambako kote huko mwezi haujaonekana.
Aidha Muft ametumia nafasi hiyo kuwatakia waislamu wote maandalizi mema ya Eid Fitr huku akiwakaribisha kwenye Baraza la Eid litakalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.