ZINAZOVUMA:

Mtaala mpya wa elimu kuibua vipaji

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema inaboresha mitaala ya...

Share na:

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema kuwa mapitio ya mitaala ambayo yataongeza masomo na kozi mbalimbali zilizojikita kutoa zaidi ujuzi utakaowawezesha wahitimu kujiajiri.

Aidha imepokea ushauri wa Mbunge wa Viti Maalum, Naghenjwa Kaboyoka ya kutumia bidhaa zinazotokana na ubunifu wa wanafunzi kuviingizia vipato vyuo na shule.

Katika Swali lake la msingi, Mbunge huyo aliitaka kufahamu endapo serikali inaona umuhimu wa kuanzisha masomo yatakayoibua vipaji vya watoto.

Akijibu Swali hilo Bungeni, Dodoma leo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema: “Serikali inatambua umuhimu wa masomo yanayoibua vipaji vya watoto kuanzia ngazi ya Elimu ya Msingi.
“Kwa kuliona hilo Wizara ilianzisha somo la Sayansi na Teknolojia kuanzia Darasa la Tatu, Stadi za kazi pamoja na Sanaa na Michezo.”

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya