ZINAZOVUMA:

Msumbiji yaingia makubaliano na Tanzania

Tanzania na Msumbiji zaingia makubaliano ya kushirikiana katika kuendeleza vitalu...
Ruvuma Basin image

Share na:

Serikali ya Msumbiji kupitia National Institute of Petroleum (INP), imeingia makubaliano ya kushirikiana kwenye gesi na Serikali ya Tanzania.

Katika makubaliano hayo serikali ya Tanzania, imewakilishwa na Mamlaka ya udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA).

Akubaliano hayo ni kwa ajili ya kupata muafaka wa kuvuna gesi inayopatikana mpakani mwa nchi hizo mbili.

Mataifa hayo yanatarajia kutumia mfumo wa unitization, katika kuendeleza vitalu vilivyopo katika mpaka wa Tanzania Na Msumbiji.

Unitisation” ni mchakato wa kuendeleza vitalu vya mafuta au gesi kwa leseni zaidi ya moja, huku wamiliki wakishirikiana katika kuendeleza.

Sababu kubwa ya kutumia mfumo huu, ni hali ya kijografia ambapo baadhi ya vitalu vimevuka mipaka ya Tanzania.

Na vikiendelezwa na upande mmoja gesi au mafuta yote yanaweza kunyonywa na upande huo, bila kufaidisha upande wa pili.

Hivyo ili kufaidisha pande zote mbili nchi hizo zimeingia makubaliano hayo, na wamiliki wa vitalu hivyo watashirikiana.

Hata hivyo makubaliano hayo hayako wazi juu ya namna watakavyoshirikiana kwenye ghrama za kuendeleza vitalu hivyo, ila yanasema watashirikiana kwa usawa.

Tayari zimegundulika “TCF” 172 za gesi katika vitalu viwili 5/A na 5/B, na vitalu 4/A na 4/B vimeonesha kuingia upande wa Msumbiji kutokea Tanzania.

TCF 172 – 172 Trillion Cubic Feet – Futi za Ujazo Trilioni 172

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya