ZINAZOVUMA:

Msiwe kama wale, wanatuharibia sana- Sheikh Twaha Bane

Sheikh Twaha Bane amewataka Mahujaji kutimiza ibada hiyo kwa nia...

Share na:

Imeandaliwa na Selemani Magali

Zikiwa zimebaki siku nane kufika siku ya mwisho ya kukamilisha mikataba ya nyumba na huduma zingine kwa mahujaji watarajiwa, mlinganiaji wa siku nyingi wa dini ya Kiisma Sheikh Twaha Bane amewataka Mahujaji kutimiza ibada hiyo kwa nia thabiti badala ya kuifanya kuwa ni sehemu ya utalii na kuongeza wasifu wao.

Sheikh Bane ametoa rai hiyo hivi karibuni wakati akizungumza baadhi ya waislam waliohudhuria katika semina maalum ya mahujaji iliyoandaliwa na Taasisi ya Jamarat Hajj and Umra na kufanyika katika msikiti wa Istiqaama uliopo Karibu na uwanja wa mpira wa Karume, Jijini Dar es Salaam.

Sheikh Twaha Bane ambaye ni msomi bobevu wa dini ya Kiislam, amesema anakwazwa na vitendo vya baadhi ya mahujaji waliotekeleza ibada ya hijja mjini Makka ambao wanakuwa sababu ya watu kuona ibada hiyo haina tofauti. “Hivi karibuni tumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya mahujaji kuonekana Malaya zao wakiwa mbugani, wengine wamerudi katika kazi zao za miziki, wengine wanatangaza kamari kwa kweli hii inachafua sana hali ya hewa,” alisema Sheikh Twaha Bane

Vilevile amesema amekuwa akipokea maswali mengi kutoka kwa jamii wakihoji wanayoyanona kwa mahujaji, jambo ambalo amedai watu wengi wanaumia na vitendo vya kipuuzi vinavyofanywa na watu hao wachache. “Nawasisitiza sana juu ya kuweka nia ya kuitikia wito kwa dhati, hakika hilo ndilo jambo muhimu sana, nyie ni kati ya watu wachache ambao mmeteuliwa na Mwenyezi Mungu kuitikia wito wake, furahini,” alisema.

Pia amesema wapo viongozi wa kisiasa wanaposikia wameteuliwa katika nafasi flani mara nyingi wanafurahi, vipi leo Mungu amekuteua katika watu wake usifurahi. “Unajisikiaje kiongozi wanchi akikuteua kuwa mkuu wa mkoa? Bila shaka ungefurahi. Vipi usifurahi kwa kuteuliwa na Mungu kuitikia wito wake? aliongeza Sheikh Twaha Bane.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Taasisi ya Jamaarat Hajj and Umra Travelleres Ukht Mayasa Sadallah ametoa wito kwa waislam waliotia nia ya Hijja kuharakisha taratibu.

“Ratiba ya mwaka huu ni tofauti na miaka mingine hivyo shime waislam mfanye haraka katika malipo kwani inawezekana kabisa ukawa na fedha na ukashindwa kusafiri,” alisema Saddallah. “Sisi tayari tumeshafanya maandalizi ya awali Februari 18 tunakwenda tena kukamilisha taratibu za mikataba, ikifika Februari 25, 2024 inakuwa mwihso, hataka kama unakuwa na fedha zako hutaweza kwenda hijja,” alisema. Taasisi ya Jamarat Hajj and Umra Travellers chini ya Mwenyekiti wake, Sheikh Mussa Kundecha imekuwa na utaratibu wa kutoa semina kwa muhujaji wake mapema ili kuwandaa kutekeleza ibada ipasavyo.

Mwaka huu 2024 Tanzania ianakususdia kusafirisha mahujaji 3700, idadi hiyo ikifikiwa itakuwa ni hatua kubwa imepigwa na taifa la Tanzania kwani malengo makubwa ya taifa ni kufikisha idadi ya mahujaji 25,000 lakini kwa miaka mingi hatujafanikiwa.

Mafanikio makubwa yalifikiwa mwaka 2023 ambapo Tanzania iliweza kuandikisha idadu ya mahujaji 3,100 na kuwapeleka Makkah kwenda kutekeleza ibada ya hijja.

Mwaka 2024, Taasisi ambazo zimeruhusiwa kuratibu safari za hijja ni pamoja na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), Ahal-Daawa, Jamaarat, Peace Travel, M2 travel, Ibn Batuta, Zamzam Centre, Muslim Hajj Trust, Alhusna Hajj Trust na Manaski Hajj.

Zingine ni Masjid Al-dir, Furkaan Hajj and Umra, Ajuwa Hajj and Travel agency, Al-Hashm agency for Hajj and Umra, Safwa Travel, Atwaif Hajj and Umra, Al-Kheibar Hajj and Umra, Joofu Hajj and Umra, Nasiha Hajj and Travel Agency, Muswafi Hajj, Sagafu Hajj and Umra, Jasuta Hajj and Umra, Masjid Jabar Hilla, I travel Hajj and Umra na Uhudi Hajj Travel.

Ratiba inaonyesha Februari 25, 2024 ni siku ya mwisho ya kukamilisha mikataba ya nyumba na huduma zingine kwa nchi zinazotegemea kupeleka mahujaji. Hakuna nafasi nyingine itakayotolewa kwa watu ambao hawatakamilisha mikataba yao ya nyumba kwa ajili ya wageni wao.

Machi 5, 2024 itakuwa ni mwanzo wa kutoa viza kwa mahujaji wote watarajiwa, wakati huo huo siku ya mwisho ya kutoa viza kwa mahujaji itakuwa ni April 29, 2024.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya