Leo tarehe 9 Aprili 2023 yamefanyika mashindano ya 23 ya Quran Afrika yaliyofanyika uwanja wa Uhuru na kuandaliwa na taasisi ya Al hikma foundation chini ya uongozi wa Sheikh Nurdin Kishk.
Mashindano hayo yameshirikisha nchi ishirini kutoka Afrika na washiriki maalumu watatu kutoka Saudi Arabia, Marekani na uingereza.
Mshindi wa mashindano hayo ni Omar Mohammed Hussein Kutoka Misri ambae amejishindia pesa taslimu shilingi milioni 23, mshindi wa pili ni Cheikh Mouhadou Mahi kutoka Senegal ambae amejishindia pesa shilingi milioni 15, na mshindi wa tatu ni AbdulRaheem Abubakar Kutoka Tanzania ambae amejishindia shilingi milioni 10.
Huku kijana mdogo zaidi katika mashindano hayo ni Swalahuddin Kateregga mwenye umri wa miaka 13 kutokea uganda ambae amezawadiwa pesa shilingi milioni moja.
Mashindano hayo yalihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kidini na kisiasa huku mgeni rasmi akiwa ni Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt Hussein Ally Mwinyi.