Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali inatarajia kubadilisha jina la hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe na kuitwa Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili (National Instititue for Mental Health).
Waziri Ummy amesema hayo kwenye semina maalum iliyoandaliwa kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupata elimu ya masuala ya afya ya akili, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja na Bohari ya Dawa (MSD)
Waziri Ummy Mwalimu amesema kubadili jina la hospitali ya Mirembe lengo ni kujenga taswira mpya ndani ya jamii kwenye huduma zinaotolewa pale.
“mtu anaweza kwenda pale kutibiwa hata Malaria, lakini jamii inamuita ‘chizi'”.
“Tunataka Hospitali ya Mirembe ifanye kampeni za hamasa na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya afya ya akili, matibabu, tafiti mbalimbali za masuala ya afya ya akili pamoja na kufanya mafunzo.