ZINAZOVUMA:

Messi asimamishwa PSG

Lionel Messi amesimamishwa kwa muda wa wiki mbili kwa kosa...

Share na:

Klabu ya Paris Saint Germain PSG imemsimamisha nyota wake raia wa Argentina Lionel Messi kwa muda wa wiki mbili kwa kosa la kuondoka kambini kwenda kwenye biashara zake binafsi nje ya jiji la Paris.

Mchezaji huyo alikosa mazoezi siku ya jumatatu na wachezaji wenzake na taarifa zinasema kwamba yupo nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kufanya tangazo la kibiashara.

Picha mbalimbali za nyota huyo alizo tupia katika mtandao wake wa Instagram zilimuonesha akiwa na familia yake nchini humo lakini pia waziri wa utalii nchini Saudi Arabia aliandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa ana furaha kumkaribisha Messi na familia yake.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 sasa, anatarajia kumaliza mkataba wake na klabu yake ya PSG June 30 mwaka huu na taarifa zinasema huenda asiendelee kubaki tena katika klabu hiyo.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya