Ligi kuu nchini uingereza EPL imesema mechi zitakua zikisimama ili kutoa nafasi kwa wechezaji walio katika funga waweze kufuturu.
Ligi hiyo imewapa ruhusa waamuzi kusimamisha mchezo muda wa kufuturu unapofika ili kuwapa nafasi wachezaji watakao kuwa katika swaumu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Ibada hiyo ya funga inatarajiwa kuanza ndani ya wiki hii na miongoni mwa wachezaji maarufu wa ligi hiyo ni waislamu na wanatarajiwa kufunga, ikiwemo Mohammed Salah wa Liverpool, Ngolo Kante wa Chelsea, Riyard Mahrez wa Manchester city na wengine wengi.