ZINAZOVUMA:

Mbunge Kenya ashutumiwa kuunga mkono Palestina

Mbunge Farah Maalim wa Dadaab apingwa vikali na wabunge wenzie...

Share na:

Farah Maalim mbunge wa Dadaab nchini Kenya, amejikuta katika wakati mgumu, baada ya kuvaa kilemba maarufu kama ishara ya Palestina.

Mbunge huyo alivaa kilemba hicho, kama ishara ya kutokuunga mkono mashambulizi dhidi ya Gaza huko Mashariki ya Kati.

Bwana Farah ameshajihisha nchi mbalimbali kuunga mkono katia changamoto zinazowakuta kutokana na mashambulizi ya Israel.

Hata hivyo, baada ya mbunge huyo kuvaa kilemba hicho, wabunge wenzake wa bunge la Kenya wamemtuhumu kwa kutokuzingatia kanuni za Bunge.

Mbunge huyo alitinga kilemba chake hicho, siku chache baada ya serikali ya Kenya kukamata watu kadhaa kwa wanaohisiwa kuhusika na mkusanyiko wa wafuasi wa Palestina, Jijini Nairobi.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya