ZINAZOVUMA:

Mamia wafariki kwa kipindupindu na homa ya denge Sudan

Watu wengi wamepoteza maisha kutokana na mlipuko wa kipindupindu na...

Share na:

Mlipuko wa homa ya Denge na Kipindupindu uliotokana na ukosefu wa maji umeua mamia ya watu katika taifa la Sudan huku ripoti za wataalamu wa afya zikitoa onyo kwa mlipuko huo kusambaa zaidi.

Chama cha madaktari wa Sudan kimeonya kwamba hali ya afya katika jimbo la kusini mashariki la Gedaref, kwenye mpaka na Ethiopia, imekuwa mbaya kwa kiwango kikubwa ambapo maelfu wameambukizwa homa ya Denge.

Japokuwa Gedaref haijapata athari za moja kwa moja za vita baina ya jeshi na vikosi vya akiba vya (RSF) lakini imekubwa na mgogoro kutoka kwa watu waliokosa makazi na huduma za kibinadamu.

Zaidi ya miezi mitano katika vita, asilimia 80 ya hospitali za Sudan hazifanyikazi kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Hata kabla ya vita, sekta ya afya isiyo madhubuti ilikuwa na wakati mgumu kukabiliana na milipuko ya magonjwa ya kila mwaka inayo endana na msimu wa mvua kuanzia Juni ikijumuisha na Malaria na Denge

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya