ZINAZOVUMA:

Makamu wa Rais ataka vijana wachangamkie fursa

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango amewataka vijana...

Share na:

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kujipatia kipato pamoja na kukuza pato la nchi.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo ya Nanenane jana Agosti 02, 2023 yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.

“Kwa dhati kabisa namshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu kwa uamuzi wake wa kutoa msukumo katika uwezeshaji wa vijana kupata ajira kupitia miradi ya jenga kesho iliyo bora (Building a Better Tomorrow – BBT), kwa upande wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Hivyo, nawasihi vijana kuchangamkia fursa hizi ili kujipatia ajira na kukuza uchumi wao binafsi na wa Taifa kwa ujumla,” amesema.

Aidha, amesema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kuongeza uzalishaji, tija na thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na kukuza kipato na kutoa ajira kwa wananchi

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya