ZINAZOVUMA:

Mahakamani kwa kudanganya uraia apate kitambulisho cha nida

Raia wa Marekani afikishwa mahakamani kwa kudanganya uraia ili aweze...

Share na:

Raia wa Marekani aliyefamika kwa jina la Yaki Juma amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka matano ikiwemo kutoa taarifa za uongo na kujipatia kitambulisho cha taifa.

Juma alisomewa mashitaka yake jana na wakili wa serikali, Godfrey Ngwijo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi.

Katika shitaka la kwanza, Ngwijo alidai Septemba 14, 2023 katika Ofisi za Uhamiaji Ilala, Dar es Salaam, mshitakiwa huyo alibainika akiishi nchini bila kibali.

Katika shitaka la pili alidai kuwa katika tarehe hiyo na eneo hilo, mshitakiwa huyo akiwa raia wa Marekani, alitoa taarifa za uongo kwa maofisa uhamiaji kuhusu utaifa wake kwa lengo la kujipatia hati ya kusafiria ya Tanzania.

Katika shitaka la tatu alidai kuwa katika tarehe hiyo na eneo hilo, Juma aliwasilisha nyaraka za kughushi kwa lengo la kujipatia cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha taifa la Tanzania.

Katika shitaka la nne alidai kuwa mshitakiwa huyo alitoa taarifa za uongo kuhusu uraia wake kwa lengo la kujipatia kitambulisho cha taifa.

Katika shitaka la tano inadaiwa kuwa mshitakiwa huyo alifanikiwa kupata kitambulisho cha taifa la Tanzania kwa njia ya udanganyifu.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya